Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: televisheni ya Alalam imetangaza habari hiyo ikisema kuwa magaidi mbalimbali 119 wajisalimisha kwa jeshi la Syria katika mkoa wa Hamswi
Watu hao walijiunga na vikundi vya kigaidi nchini humo kwaajili ya kufanya jiadi ama kutokana na hali iliopo ndani ya nchi hiyo wameamua kujisalimisha kwa jeshi la nchi hiyo kwaajili ya kutafuta suluhu na mani nchini humo.
Mpaka sasa magaidi wengi wamejisalimisha baada ya kugundua kile walichokuwa wakidanganywa kuwa wanaenda kupigana jiadi, hali yakuwa si kweli kuwa ni jiadi, hivyo kuamua kujisalimisha kwa majeshi ya Syria.
Aidha televisheni ya Alalam aliongeza kusema kuwa: kutokana na athari ya mapambano hayo makali baina ya magaidi na majeshi ya Syria katika kijiji cha (Sanisel) kiliopo kaskazini mwa mkoa wa Humeh na Hamswi ambapo imepelekea kuangamia idadi kubwa ya magaidi hao.
Mkoa wa Halab ndio mkoa mkubwa zaidi nchini Syria ambapo kwa upande wa mashariki umepakana na nchi ya Iraq na kwa upande wa magharibi umepakana na nchi ya Lebanon.
Asilimia tisini ya mkoa huo mpaka sasa uko mikononi mwa majeshi ya Syria, isipokuwa imebaki sehemu ndogo ya upande wa kusini na kaskazini mwa mkoa huo ikiwemo wilaya ya kale ya Palmyra na Al-Qaryatayn na boda ya Abulwalid iliopo mpaka na Iraq ambapo ziko chini ya magaidi wa Daesh.
Mwisho wa Habari/290